Hii ni moja kati ya taarifa ambazo nimeona umuhimu wake na kuipa nafasi
kama ilikupita mtu wangu, ni kuhusu habari iliyoandikwa na gazeti la Habari leo
kwamba kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation ya Beijing,
imesema iko tayari kuja Tanzania kuijenga upya reli ya kati , ambayo kwa sasa
imechakaa na inashindwa kuhimili shehena kubwa ya mizigo kuwa ya kisasa.
Injini na Mabehewa ya reli hiyo kongwe Tanzania
vimechakaa wakati ni tegemeo kubwa kwa wakazi wengi wa baadhi ya mikoa ya Tanzania na pia
ni sehemu nyingine ya kuukuza uchumi wa nchi.
Rais
wa kampuni hii ya China amemwambia Waziri mkuu kwamba tayari wameanza
mazungumzo na Wizara ya uchukuzi na kama watakubaliana, wako tayari kuja Tanzania na kuijenga hii reli ikiwa ni kampuni
ambayo pia iliijenga reli ya Tazara baada ya Hayati Mwalimu Nyerere kuiomba
serikali ya China.
kufumua reli yote kutoka Dar es salaam mpaka Kigoma na Mwanza ila
watafanya kwa awamu ili usafirishaji wa abiria na mizigo uendelee wakati huohuo
ujenzi ukiendelea Amesema pia ujenzi wa kiwango hicho kinachotakiwa ni gharama
na hawawezi.
Waziri mkuu Mizengo Pinda alisema kuna kampuni kadhaa kutoka mataifa mbalimbali
ambazo zimeonyesha nia ya kujenga reli hiyo lakini waliona wawasiliane na China kwanza
ambayo kuna historia ya ushirikiano mzuri.
Kutokana na uchakavu wa hii reli ya kati, kiwango cha kusafirisha
mizigo ya ndani na nje ya nchi kimeshuka ambapo siku za safari za treni ya
abiria zimeshuka kutoka safari saba kwa wiki mpaka safari mbili kati ya Dar es
salaam, Mwanza na Kigoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni