Amekua mtu wa kumiliki headlines kila
anapokanyaga sasa hivi na tena uzito umeongezeka baada ya kuwekwa hadharani kwa
uhusiano wake wa kimapenzi na TV Star Kim Kardashian.
Rapper Kanye West mwenye umri wa miaka 36
akiwa kwenye Tour yake ya ‘Yeezus’ alifanya watu wengi wazitumie sana camera zao kutokana na aina ya ubinifu uliotumiwa
kwenye show yake huko Seattle
Marekani.
Unaambiwa baadhi ya matukio ya show hii kwenye crowd ya zaidi ya watu
elfu 17 ni wakati pia alipofanya show akiwa kwenye sehemu zilizotengenezwa kama
milima lakini pia ambacho kilifanya camera za fans zitumike sana ni pale
alipofanya show huku kwenye stage akiwa amepanda mtu anaefanana na Yesu, huyu
ni mtu ambae tayari alikua ameandaliwa kwa ajili ya hii show ambayo set yake
ilikua designed na kampuni ya Kenye, Donda Creative.
Kanye na mikono ya Mashabiki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni