Standard Media wametoa taarifa nyingine ambayo inazidi kulipa shambulio
la Westgate nguvu ya kuendelea kumiliki vichwa vya habari baada ya kuripoti
kwamba Magaidi waliofanya hilo shambulio Nairobi mwezi September walitumia helikopta ambayo
inamilikiwa na mwanasiasa maarufu wa zamani nchini Kenya ambae taarifa hii haijamtaja.
Imefahamika, sita kati ya magaidi walitumia helikopta hiyo kutoka
kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab
mpaka Nairobi
kwa kuhofia kushtukiwa mapema na kukamatwa iwapo wangetumia usafiri wa ardhini.
Wapelelezi wamesema wanaamini kwenye helikopta hiyo, magaidi hawa
walibeba baadhi ya silaha za kivita ambazo zilitumika kwenye shambulio hili
ambalo liligharimu maisha ya zaidi ya watu 60 akiwemo ndugu wa Rais Uhuru
Kenyatta.
Magaidi hawa wanaaminika kuingia kwenye kambi ya Dadaab wakitokea Somalia miezi
sita iliyopita ambapo walijifanya Wakimbizi huku wakiendelea kupanga shambulio
la September 21 ambapo baadae walichukua hiyo helikopta ambayo tayari Pilot
wake alikamatwa na kuhojiwa na kisha baadae kuachiwa.
Hata hivyo imegundulika pia ndani ya jumba la Westgate ambalo ndani
yake lina maduka na migahawa mbalimbali, kwenye floor ya kwanza kulikua na raia
wa Uturuki ambae alikodi chumba cha duka zaidi ya mwaka mmoja uliopita na
kuanza kukitumia kwa biashara ya kuuza simu miezi sita iliyopita na pia chumba
hichohicho kutumika na magaidi kama sehemu ya
kuhifadhia silaha.
Raia huyu wa Uturuki alisafiri kwenda nje ya Kenya
siku moja kabla ya shambulio la Westgate na Polisi wanaendelea na msako ambao
pia unalihusisha gari aina ya BMW ambalo lilimilikiwa na yeye na kutumika
kubeba Magaidi hawa kwenye mizunguko mbalimbali ya Nairobi.
Kwa kumalizia post hii, kingine cha kukwambia ni kuhusu Mwanamke mmoja
aliefahamika kwa jina la Wanjiru kutoka kijiji cha Kangari huko Nyeri
kugundulika kwua mmoja wa Magaidi na mpaka sasa Watu wa usalama wanandelea
kufatilia kama na yeye aliuwawa kwenye majibizano ya risasi kati ya magaidi na
vikosi vya usalama.
Kuwa mwanachama wa millardayo.com kwa kujiunga na
facebook.com/millardayo twitter.com/millardayo na instagram.com/millardayo na
kupata nafasi ya kuzipata taarifa mbalimbali pamoja na picha za matukio ya kila
aina yanayotokea Tanzania na
nje ya Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni