Msanii wa Muda sasa kwenye Industry ya
Bongo Fleva Noorah a.k.a BabaStyle amevunja ukimya kwa kuamua Kufunguka kile
kilicho moyoni mwake kuhusu ukimya wake kwenye Game kwa sasa ambapo amefika
mbali na kusema kuwa Mziki hauna faida kwake na kwa sasa anaufanya Mziki kama
Starehe like mtu anavyotoka kwenda Bar kunywa beer huku akiwa sio Mlevi means
siku akifeel ham tu.
Akizungumza
na DJ HAAZU
ndani ya Kipindi cha DUNDO ndani ya MJ
RADIO Arusha Noorah ameelezea ukimya wake ambao yuko nao kwamba Kwa
sasa mziki hautegemei tena kwamba utakuja kumpa faida kwani ameusotea kwa muda
Mrefu sana bila Mafanikio na kusema kuwa Hana time nao tena bali ana mambo
mengi ya kufanya yanayomuendeshea Maisha yake na sio muziki ila ataufanya tu
kama sehemu ya Starehe.
Amejaribu kufafanua kuhusu wingi wa
Wasanii kuwa wengi Nchini huku wenye Mafanikio wakiwa wachache ambao pia
amewataja kama watu wa kusifiwa wana hela ila
sio kiivyo ambapo wanasemwa wamefanikiwa kumbe ni maneno tu (Politics kwenye
muziki).
POINT YA NOORAH INASEMA Maisha ni
Malengo na kama kitu hakina faida nacho hakina
maana kwako
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni