Ni nadra sana kwa Mastaa wengi wa Tanzania
kukubali kusema kiwango anachopata kwa mwezi kutokana na kazi yake ya umaarufu
ila kwa Mzee Majuto ni kinyume, amekubali kusema kila kitu kwenye kipato cha
movie zake za vichekesho ambazo mpaka sasa ndio zinashika namba 1 kwa mauzo Tanzania?
Kwa sababu ni kiapo cha zamastreet.blogspot.com
kuhakikisha chochote ambacho ni stori unakipata, imempata Mzee huyu Mbembe
kutoka Kigoma akiwa ni mzaliwa wa Tanga umri ukiwa miaka 65 na kukubali
kuzungumza kwenye hii Exclusive interview.
Akiwa ni baba wa watoto tisa, anakwambia
‘kwenye movie za kuigiza sasa hivi kama mtu akitaka kunishirikisha ni lazima
unilipe milioni nane kutoka milioni 2 au tatu nilizokua nazikusanya mwanzoni,
hii bei nimeibadili kuanzia mwezi September 2013, mimi kadri ninavyocheza movie
nyingie za kushirikishwa ndio nazidi kujipunguzia kipato changu kwa mwezi
kutoka kampuni ya STEPS iliyoniajiri’
‘Mpaka sasa nimecheza movie zaidi ya 600 toka
nimeanza kuigiza za kushirikishwa na zangu mwenyewe, nilianza kulipwa zaidi ya
milioni moja kwenye movie toka mwaka 2007/2008 baada ya kuwa na kampuni ya Ally
Riyami ambae alikua ananilipa shilingi laki sita kwa kila movie ya Comedy kwa
hiyo kwa mwezi napata mpaka kwenye milioni 6 au saba kutokana na idadi ya movie
nitakazoigiza’ – Mzee Majuto
‘kwa sasa hapa Steps nalipwa kuanzia milioni
17 mpaka 20 kwa mwezi, ni malipo mazuri sana ambayo napata kila mwezi na nimepangiwa
kucheza movie 9 kwa mwaka lakini kule Ally Riyami kwa mwezi ndio nilikua
nacheza hizo movie 10, yani unacheza movie mpaka unasikia kizunguzungu…. kwa
sababu nilitakiwa kucheza movie 1 kila baada ya siku tatu ila kwa sasa kwenye
mkataba wa Steps nacheza movie moja ya kampuni na moja ya nje ya kampuni,
maisha mazuri’ – Mzee Majuto
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni